Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CCM yatoa tamko kuachiwa kwa Mbowe

Shakapicc Data Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shaka

Sat, 5 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Siku moja baada ya Mwenyekiti wa Taifa wa chama cha Chadema kufutiwa mashtaka, chama cha CCM kimesema kinatumaini huo ni mwanzo safari mpya ya kisiasa na ya kusimama kama Watanzania.

Jana Machi 4, 2022 Mbowe na wenzake watatu walifutiwa mashtaka ya ugaidi  baada ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali (DPP) kuieleza mahakama hana nia tena ya kuendelea na kesi hiyo.

Baada ya kuachiwa huru, Mbowe alikutana Rais Samia Suluhu Hassan ambapo wawili hao walikubaliana kushirikiana na Serikali katika kuleta maendeleo.

Akitoa maoni yake kuhusu hatua hiyo  leo Jumamosi Machi 5, 2022 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shaka amesema katika Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 hadi 2025, ibara ya 118, CCM iliahidi kuwa itasimamia ustawi wa demokrasia, utawala wa sheria pamoja utawala bora.

“Kwanza nampongeza mheshimiwa Mbowe kwa uungwana wake na kujali kwa kumshukuru mheshimiwa Samia na kumuahidi ushirikiano na hiyo ndio siasa siasa bora. Siasa bora ni kuheshimu utu, kuheshimiana lakini vile vile kuishi kwa amani,” amesema.

Shaka amesema hiyo ndiyo Tanzania ambayo Watanzania na dunia inahitaji kuona nyakati ambazo Rais Samia anafanya kazi nzuri ya kuifungua nchi.

Advertisement “Sisi kama chama tuahidi ushirikiano kama Rais Samia alivyomuahidi Mheshimiwa Mbowe jana CCM,  tunaahidi ushirikiano na kufanya siasa safi na za kuvumiliana lakini siasa za maendeleo na siasa za hoja kwa hoja,”amesema Shaka.

Amesema kwenye jambo hilo anawapongeza pia Watanzania kwa namna ambavyo wameonyesha uimara, mshikamano na umoja wao na kwamba hiyo ndiyo siri ya mafanikio.

“Tuna matumaini makubwa tunaenda kuianza safari mpya ya kisiasa lakini ya kusimama ya kama Watanzania. Tuna kazi moja sasa hivi ya kuleta maendeleo na kuhakikisha kuwa nchi yetu inapiga hatua. Hapa ambapo Rais Samia ametufikisha tunahitaji kwenda mbali sana kiuchumi, kijamii na kisiasa,” amesema.

Rais Samia, Mbowe wateta Ikulu

Saa chache baada ya kutoka gerezani mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amekutana na Rais Samia Suluhu Hassan Ikulu jijini Dar es Salaam. Soma zaidi

VIDEO- Kauli ya kwanza ya Mbowe akitoka gerezani

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amewaambia waandishi wa habari waliomfuata kutoka gerezani hadi nyumbani kwake kuwa sasa ni wakati wa kunyamaza, lakini atakuja kuzungumza na viongozi na baadaye vyombo vya habari. Soma zaidi

Chanzo: www.tanzaniaweb.live