Mkurugenzi Ilemela amuhakikishia Mwenezi Makonda ndani ya Wiki mbili kukarabati eneo linalotuhama maji katika stendi hiyo.
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndg. Paul Makonda kimetoa muda wa siku 4 hadi kufikia tarehe 17 Novemba, 2023 kukamilisha utaratibu wa kutoa vitambulisho kwa Mawakala wanaofanya kazi ya kutoa huduma ya mabasi katika stendi hiyo.
Hatua hiyo imekuja mara baada ya Mwenezi Makonda kuisikia na kuipokea changamoto hiyo iliyoelezaa na Mbunge wa Ilemela Mhe. Angelina Mabula na ndipo alipoifanyia kazi kwa kuitolea maelekezo ya Chama.
Pia, Mwenezi Makonda wakati akipofika katika stendi hiyo, alitembezwa na Wafabyabiashara wa hapo kujionea maji yalivyotuhama katika eneo la kuingilia katika stendi hiyo ambapo Mwenezi Makonda alimtaka Mkurugenzi wa Ilemela kuji commite mwenyewe ni lini patakarabatiwa.
Katika majibu yake, Mkurugenzi amesema Wameshatoa Tsh Milioni 468 kwa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami iliyopita hadi hapo stendi na mchakato unaendelea na kumuhakikishia Mkurugenzi kuwa ndani ya wiki mbili kuweka paving blocks pamoja na njia za kupitishia maji ya mvua katika eneo ambalo ndipo maji yanatuhama na kuweka matope.