Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CCM yatoa madai mazito jimbo la Sugu

JPM CCM5 CCM yatoa madai mazito jimbo la Sugu

Fri, 19 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

JOTO la uchaguzi Mkuu wa madiwani, wabunge na Rais limeanza kupanda mkoani Mbeya baada ya ChMadai hayo yametolewa na Katibu wa Siasa, Itikadi na Uenezi wa CCM, Bashiru Madodi, akiwa kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Mbeya jijini Mbeya.

“Tunajua kwamba kuna fedha kutoka nje ya Mkoa wa Mbeya zimeingizwa ili kuhakikisha kuwa CCM inashindwa uchaguzi hapa Mbeya Mjini, tunajua kuwa kuna wana- CCM wenzetu wameanza vikao vya siri kuwasaidia wapinzani ili washinde, niwahakikishie kuwa mwaka huu hatutawavumilia,” alidai bila kutoa uthibitisho.

Madodi aliwaagiza Wenyeviti wa CCM ngazi ya Wilaya pamoja na kamati za Siasa za Wilaya kuorodhesha majina ya wanachama wa CCM ambao wameanza vurugu za kujipitisha kwa wanachama kuomba kupigiwa kura ili wapate nafasi ya kuteuliwa kugombea ubunge na udiwani kwenye maeneo yao na kuyafikisha ofisi ya CCM mkoa ili hatua kali dhidi yao zichukuliwe.

Alisema kuwa CCM inazo taratibu zake za kufanya uteuzi wa wagombea hivyo ikitokea mwanachama anakiuka taratibu hizo ni lazima hatua kali zichukuliwe dhidi ya mwanachama huyo kwa nia ya kulinda katiba, kanuni na miongozo ya chama. “Hata sisi ngazi ya Mkoa tumeanza kuorodhesha watu ambao wameanza fujo mapema kwa ajili ya uchaguzi na hata ninyi viongozi wa CCM ngazi ya Wilaya andikeni majina ya watu wa aina hiyo na kutuletea ili tuwashughulikie kwa mujibu wa taratibu za chama chetu,” alisema Madodi.

Aliongeza kuwa, uzoefu unaonyesha baadhi ya wanachama wa CCM hasa katika Jimbo la Mbeya Mjini wasipoteuliwa kugombea nafasi za uongozi hukisaliti chama na kwenda kuwasaidia wapinzani, jambo ambalo kwa mwaka huu haliwezi kuvumiliwa hata kidogo.

Madodi alisema kuwa ikitokea mwanachama yeyote wa CCM akahisiwa au kubainika kuwa anashirikiana na wapinzani kukihujumu chama kwenye uchaguzi Mkuu ujao, atasimamishwa uanachama na baada ya uchaguzi kumalizika atashughulikiwa.

“Tukikubaini kuwa unakihujumu chama kwa kushirikiana na wapinzani wakati wa uchaguzi, tutakachokifanya kwanza ni kukusimamisha uanachama kwanza ili utupishe sisi tuendelee kukipigania na baada ya uchaguzi tutarudi kukushughulikia na niwakumbushe tu kwamba hakuna kosa kubwa kama kukifanya chama kinuke mbele ya watu au kukihujumu kwenye uchaguzi, adhabu yake ni kufukuzwa uanachama,” aliosema Madodi.

Katibu wa CCM Mkoa wa Mbeya, Solomon Itunda alisema kuwa mazingira ya uchaguzi Mkuu ya mwaka huu ni tofauti na yale ya mwaka 2015 hivyo CCM ngazi ya Mkoa imejipanga kuhakikisha inawafuatilia wanachama wote ambao watathubutu kukisaliti chama na kwenda kuwasaidia wapinzani.

Alisema kuwa chama kimeweka mikakati ya kuhakikisha CCM inashinda jimbo la Mbeya Mjini na kwamba yeyote atakayejaribu kuvuruga mikakati hiyo atashughulikiwa ipasavyo.

“Tumejidhatiti kimkakati kuhakikisha CCM inashinda uchaguzi hapa Mbeya Mjini, kwa mwanachama wetu atakayejaribu kuvuruga mikakati yetu hatutamvumilia na hakuna jiwe litabaki juu ya jiwe maana yote tutayapindua,” alisema Itunda.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya, Mchungaji Jacob Mwakasole, aliwataka wana-CCM kujenga umoja na mshikamano wakati wote wa mchakato wa uchaguzi Mkuu ili kuhakikisha chama hicho kinapata ushindi wa kishindo katika ngazi zote.

Mchungaji Mwakasole alisema njia pekee ya kuifanya CCM ishinde uchaguzi ujao ni kuwafanya wanachama pamoja na wananchi wote kuwa wamoja kwa kujenga mshikamano ambao utaihakikishia CCM ushindi katika ngazi zote za udiwani, ubunge na Rais.

Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015 hadi 2020 mkoani Mbeya, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila, alisema zaidi ya Sh. bilioni 227 zimetolewa na Serikali Kuu kwa ajili ya miradi ya maendeleo pekee mkoani Mbeya.

Alisema kuwa fedha hizo zilitolewa ndani ya kipindi cha miaka mitano iliyopita na kudai kuwa sekta iliyoongoza kwa kupata fedha nyingi ni barabara ambayo ilipewa zaidi ya Sh. bilioni 85 kupitia kwa Wakala wa Barabara nchini (Tanroads).

Jimbo la Mbeya Mjini kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita limekuwa likishikiliwa na CHADEMA kupitia kwa Mbunge Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la Sugu.

Aidha katika kipindi cha miaka mitano iliyopita Halmashauri ya Jiji la Mbeya ilikuwa chini ya Chadema, baada ya chama hicho kunyakua viti vingi vya udiwani katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 hali ambayo imekuwa ikikinyima usingizi Chama Cha Mapinduzi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live