Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CCM yatamba kwa 'style' hii maboresho bandari kuu

Bandari DSM Ccm CCM yatamba kwa style hii maboresho bandari kuu

Wed, 8 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama cha Mapinduzi CCM, kimesema kuwa katika miaka 60 kimeweza kuongeza upakuaji wa shehena bandari kuu sambamba na kufanya maboresho ya gati jambo ambalo limechochea ongezeko la meli na ukuaji wa uchumi nchini.

Haya yamewekwa bayana na Katibu Mkuu wa CCM taifa, Daniel Chongolo mapema Desemba 08, 2021 wakati wa mkutano wa chama hicho na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Chongolo amesema kuwa mwaka 1961 wakati wa uhuru, Tanzania ilikuwa na uwezo wa kupakua shehena 118,500 pekee na kuwa hivi sasa jumla ya shehena 17,716,290 zinapakuliwa katika bandari kuu ya Dar es Salaam.

Ameongeza kusema kuwa hali hiyo imepelekea meli kubwa kuendelea kuongezeka nchini jambo ambalo limeifanya Serikali kuongeza gati na maegesho ya meli kubwa katika bandari kuu.

Amefafanua kuwa ongezeko hilo limetoa fursa kwa meli kubwa kushusha mizigo nchini sambamba na kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi nchini.

Itakumbukwa kuwa Desemba 04, 2021 Rais Samia alizindua matumizi ya gati saba zilizoongezwa kina katika bandari kuu ya Dra es Salaam jambo ambalo sasa litaruhusu meli zote kubwa kutia nanga nchini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live