Mon, 23 Jan 2023
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Geita, kimeutaka uongozi wa Halmashauri ya Mji wa Geita kuimarisha usimamizi wa miradi inayojengwa kwa mfumo wa ‘Force Account’, ili ikamilike kwa kiwango.
Mwenyekiti wa CCM wilayani Geita, Barnabas Mapande ametoa maelekezo hayo katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Geita.
Amesema mbali na serikali ya CCM kuruhusu miradi kutekelezwa kwa ‘force account’, ili mafundi wazawa wapate ajira na kunufaika moja kwa moja na miradi hiyo, lakini ni vyema usimamizi wa miradi uimarike.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live