Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CCM yashinda ubunge Amani

EF473358 740E 4B48 880B F68351F9DE0E.jpeg Mbunge mteule wa Amani, Abdul Yussuf Maalim (katikati) baada ya kuitangazwa kushinda nafasi hiyo

Sun, 18 Dec 2022 Chanzo: Mwananchi

Msimamizi wa uchaguzi mdogo Jimbo la Amani, Zanzibar, Safia Idd Muhammed amemtangaza mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdul Yussuf Maalim kuwa mshindi wa ubunge wa jimbo hilo.

Safia alimtangaza Maalim kushinda nafasi hiyo Jumamosi Desemba 17, 2022 usiku katika ukumbi wa Judo Aman.

Amesema kuwa mshindi huyo amepata kura 4, 242 sawa na asilimia 84.1 akifuatiwa na mgombea wa ACT Wazalendo, Mohamed Khamis Mohamed aliyepata kura 728 sawa na asilimia 14.4.

Uchaguzi huo umejumuisha vyama 14 vya siasa, kufuatia kifo Cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Mussa Hassan Mussa kilichotokea Oktoba mwaka huu kisiwani humo. "Kwa mamlaka niliyopewa namtangaza Abdul Yussuf Maalim kuwa mshindi wa jimbo la Aman," amesema

Awali msimamizi msaidizi wa uchaguzi, Ali Idorous Suleiman alisema idadi ya watu waliojiandikisha ni 9,919, waliopiga kura ni 5,126 na kura halali ni 5,042 na kura 84 zimekataliwa.

Naye mbunge mteule Maalim ameshukuru kwa ushindi huo huku akiahidi kushirikiana na wananchi kutatua changamoto za jimbo hilo.

Wagombea udiwani CCM Tanga washinda

Katika uchaguzi mdogo wa madiwani, wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kata mbili zilizoko mkoa wa Tanga wameibuka washindi.

Simba Kayaga wa (CCM) ameshinda udiwani kata ya Mnyanjani jijini Tanga huku Marry Mntambo akishinda nafasi hiyo kata ya Vibaoni wilayani Handeni mkoani humo.

Chanzo: Mwananchi