Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CCM yashinda kata ya Mawenzi

11558 MAWENZI+PIC TanzaniaWeb

Mon, 13 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Moshi. Mgombea wa CCM Kata ya Mawenzi, Apaikunda Naburi ametangazwa kuwa mshindi baada ya kuwashinda Afrikana Mlay wa Chadema na Isaac Kareti wa Chama cha Sauti ya Umma (Sau).

Naburi aliyepata kura 400 kati ya kura 569 alikuwa diwani wa kata hiyo mwaka 2010 hadi 2015.

Akitangaza matokeo hayo leo jioni Jumapili Agosti 12, 2018 msimamizi wa uchaguzi, Erasmo Silayo amesema mgombea wa Chadema amepata kura 163 huku Kareti akipata kura mbili.

“Idadi ya wapiga kura  waliojiandikisha ilikuwa ni 1,821, kati yao idadi halisi ya wapiga kura ni 569 na kura 4 ziliharibika,” amesema Silayo.

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz