Dar es Salaam. Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Zanzibar Dk Abdalla Juma Saadala amesema ingawa Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Abeid Amani Karume alifariki miaka 48 iliyopita, mawazo yake bado yanaishi.
Dk Sadalla amesema hayo leo Jumanne, April 7, 2020 wakati wa akizungumzia kumbukizi ya kifo cha kiongozi huyo visiwani Zanzibar.
“Alikuwa na sifa ya kujishusha na sifa ya kutawala katika Serikali shirikishi, kwa hiyo leo ni siku muhimu sana kwetu ni kweli hayupo lakini mawazo yake na hekima zake zinaendelea kudumishwa milele na milele,” amesema Dk Abdalla.
Amesema hayati Karume ni kati ya viongozi walioithibitishia dunia kwamba Waafrika wanaweza kujitawala.
“Amethibitisha kuwa sisi Waafrika, tunaweza kuungana na kujitawala, kuweka uchumi wa Taifa na kudumisha Amani na umoja wa nchi yetu,” amesema.
Kiongozi huyo wa CCM Zanzibar amesema Karume alisaidia kuleta maendeleo ya Zanzibar na alitamani kuona kila mwananchi anafaidika na matunda ya nchi yake.
Pia Soma
- VIDEO: Karume alivyopigwa risasi hadharani
- Miaka mitatu Tanzania yapoteza lita bilioni 1.4 za petroli, kodi
- Ripoti ya CAG yabaini madudu katika taasisi za umma
“Aliacha usia mzuri na viongozi wengine waliofuatia wamekuwa wakitekeleza awamu kwa awamu kwa hekima kubwa sana.”