Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CCM yasema Samia mbobezi wa uchumi

C77b3eec6e21c3144a73caea5226eeb7.jpeg CCM yasema Samia mbobezi wa uchumi

Mon, 16 Aug 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka amesema Rais Samia Suluhu Hassan anajua vizuri Tanzania inatakani na msomi aliyebobea kwenye maendeleo ya uchumi, hivyo hivyo ataivusha nchi kutoa ilipo na kwenda hutua mbele zaidi za maendeleo.

Alisema hayo jana katika ibada ya kuweka wakfu na harambee ya jengo la utawala na Shule ya Biblia, jijini Dar es Salaam.

Shaka alikuwa mgeni rasmi katika ibada na harambee hiyo iliyofanyika kwenye Kanisa la

Pentacostal Moto Moto lilipo Boko, Kinondoni, Dar es Saalam.

Katika shuhuli hiyo, Rais Samia alichangia Sh milioni 10 kuunga mkono jitihada za kanisa hilo, ambapo jumla ya Sh milioni 24 zilichangwa na waumini wa kanisa hilo.

Shaka alisema Rais Samia ameudhihirishia umma ndani na nje ya nchi kuwa anaielewa nchi anayoiyongoza, ana washauri mahiri wenye weledi, na ameweka mbele maslahi ya taifa.

“Niwahakikishie Watanzaia kupitia mkusanyiko huu kuwa, Rais Samia ni msomi mzuri katika maendeleo ya utawala na uchumi ambaye ametumikia na kushika

nyadhifa mbalimbali za kiserikali pamoja na mashirika ya kitaifa na kimataifa duniani,” alisema.

Alisema Rais Samia ni bingwa na anatosha kuivusha nchi kama alivyoweza kulivusha taifa katika nyakati ngumu katika historia ya nchi.

Alisema Rais Samia katika kuthibitisha kabobea kwenye uchumi aliielekeza Benki Kuu Tanzania (BoT) ihakikishe masharti na riba za mikopo katika benki za kibiashara vinapungua hivyo muda mfupi ujao Watanzania watarajie kuona mabadiliko katika ukuaji wa uchumi.

Shaka alisema milango ya uchumi wa nchi imeendelea kufunguka ndiyo maana

jumuiya, mashirika, taasisi na wafanyabisahara wakubwa wa kitaifa na kimataifa wameendelea kuja kuwekeza Tanzania.

“Hii ndio faida kubwa ya kuwa na Rais anaeijua nchi yake, anaejua anaowaongoza wanahitaji nini, kwa wakati upi na yeye asimame katika mlengo upi bila ya kuyumbishwa na mikingano ya ndani na nje. Rais Samia amekamilika kwa kila sifa ambayo dunia ya leo inauhitaji kuwa wa Rais wa nchi wa aina yake, niseme tena Tanzania Mwenyezi Mungu ametubariki,” alisema.

Shaka aliwahakikishia viongozi wa dini kuwa serikali za CCM Tanzania Bara na Zanzibar

zitaendelea kuheshimu na kuthamini jitihada za waumini wa dini zote katika kuliimarisha taifa kiimani na kimaendeleo.

“Hivyo niwasihi waumini na Watanzania wote kuendelea kuheshimiana na kuvumiliana kwenye tofauti za kidini zinazojitokeza ili kuendelea kudumisha amani na utulivu hapa nchini. Pamoja na kuendelea kukumbushana kuwa amani na utulivu ni sehemu ya kichocheo kikubwa cha maendeleo ya taifa, hivyo ni vyema viongozi wa dini kuendelea kuhubiri amani kwa waumini wenu ili iendelee kudumu” alisema.

Askofu Mkuu wa Kanisa la Pentecostal Moto Moto,

Ezra Matamya aliipongeza serikali kwa kusimamia uchumi na kwamba wanaunga mkono dhamira ya serikali ya kulinda haki na Katiba.

Alisema Watanzania wengi wana imani na serikali na kwamba kuimarika kwa diplomasia ya kimataifa kunaleta fursa nyingi za ajira na uwekezaji.

Pia aliipongeza serikali kwa uamuzi wa hekima kuhusu chanjo ya corona na kutoa chanjo kwa hiyari.

“Baraza la Maaskofu lina imani kubwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwamba ataiongoza nchi kwa haki, amani na utulivu ni tunu ya tAifa hili, tunaomba jambo hili lidumishwe,» alisema Askofu Matamya.

Chanzo: www.habarileo.co.tz