Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CCM yasambaza wabunge wake kata zote jimboni Monduli

15548 Pic+ccm TanzaniaWeb

Tue, 4 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Monduli. Chama Cha Mapinduzi (CCM)kimetamba kuibuka na ushindi wa ubunge wa Monduli, asubuhi na mapema ya Septemba 16, 2018 kutokana na mikakati yake imara, ikiwemo kuhakikisha kata zote wanakuwepo wabunge kusimamia kampeni na kura.

Akizungumza na Mwananchi, Meneja Kampeni wa CCM, William Ole Nasha, amesema wana uhakika wa ushindi katika jimbo la Monduli tofauti na baadhi ya watu wanavyodhani kuwa upinzani una nguvu.

"Tumejipanga vizuri, kata zote za Monduli karibu 16 kutakuwa na wabunge na viongozi wa CCM wakiratibu kampeni na kura, lakini pia wananchi wametambua makosa waliyofanya mwaka 2015 na sasa wanataka kurekebisha," amesema.

Nasha ambaye pia ni Naibu Waziri wa Elimu, amesema katika kampeni wanazofanya tofauti na vyama vingine, CCM inasikiliza kero, kutoa ahadi na kuzifanyia kazi.

"Ndio sababu kwenye kampeni tunawaita mawaziri waje kusikiliza kero na kuzitatua tofauti na wenzetu ambao wanataka kura za kulinda heshima na si kuwasaidia wananchi kukabiliana na umasikini," amesema.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni katika kata ya Makuyuni, mgombea wa CCM, Julius Kalanga aliwataka wananchi kupuuza maneno ya upinzani kuwa alinunuliwa na ndio sababu amejiunga na CCM.

"Mimi nimejiuzulu kujali maslahi mapana ya wananchi wa Monduli, hivi ubunge una faida gani kama siwezi kutatua kero zenu, Mbunge siwezi hata kumuwekea dhamana polisi mpiga kura wangu, huu ni ubunge wa aina gani," alisema.

Alisema wanaompinga kwa kuunga mkono, serikali ya Rais John Magufuli hata wao, tayari walikwenda Ikulu na kueleza kumuunga mkono Rais Magufuli.

“Wao wanakwenda Ikulu kumuunga mkono Rais kwanini mimi wananikataza?" Alihoji Kalanga.

Chanzo: mwananchi.co.tz