Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CCM yapitisha watatu kuwania udiwani Kilimanjaro

12452 Pic+ccm+kili TanzaniaWeb

Fri, 17 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Moshi. Halmashauri ya CCM mkoani Kilimanjaro imepitisha majina matatu ya wanachana wa chama hicho watakaogombea udiwani katika uchaguzi mdogo kwenye kata tatu zilizo wazi.

Katibu wa CCM mkoa huo, Jonathan Mabhia amesema kampeni zitaanza Agosti 24, 2018, huku akiwataja wagombea kuwa ni Yohana Laizer, Kia wilaya ya Hai, Robbison Kimaro- Uroki wa wilaya ya Hai na Solomon Mmary wa Nasai wilayani Siha.

Mabhia amesema wananchi wanaendelea kuiamini CCM pamoja na kuendelea kukipigia kura kwa kuwa ndicho chama ambacho kimekuwa kikitekeleza sera zake kikamilifu.

Amesema ni vyema zikafanyika kampeni za kistaarabu kwa kutangaza sera za chama na si kutukana matusi na kufanya vurugu wakati wa kampeni.

Kwa upande wake, Katibu wa Chadema mkoa huo, Bazil Lema, amesema watasimamisha  wagombea katika kata hizo na kwamba wataendelea kunadi sera za chama hicho.

“Kwa kuwa wao ndio wenye nguvu ya kupiga kunyangany’a na kuendelea kumdanganya Rais sisi hatuwaogopi, tutaendelea kuweka wagombea na kunadi sera za Chadema,”amesema Lema.

Amewaomba wananchi waendelee kukiamini chama hicho kwa kukipigia kura na kwamba wasikate tamaa kwa kuwa wanaibiwa na kunyanganywa kwa makusudi ushindi.

Chanzo: mwananchi.co.tz