Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CCM yapita bila kupingwa kata mbili Serengeti

11629 Udiwani+pic TanzaniaWeb

Tue, 17 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Serengeti. Wagombea wa udiwani wa Ikoma na Manchira wa CCM wametangazwa rasmi kupita bila kupingwa.

Msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la Serengeti mkoani Mara, Juma Hamsini amesema amelazimika kuwatangaza baada ya kuzingatia taratibu zote za kisheria ya uchaguzi.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini mwake leo Julai 17, Hamsini amesema Ikoma mgombea pekee ni Michael Kunani (CCM) baada ya mgombea wa Chadema Kennedy Josephat kushindwa kuwasilisha fomu yake kwa msimamizi msaidizi wa uchaguzi.

Kuhusu kata ya Manchira, amesema mgombea mteule wa CCM, Charles Muyuga hana mpinzani baada ya yule wa Chadema, Timani Shaweshi kubainika alidanganya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakati wa ujazaji wa fomu.

Amesema Shaweshi katika fomu amejaza hajawahi kushtakiwa lakini katika maelezo ya pingamizi alilowekewa alikiri kushtakiwa mwaka 2008 kwa kosa la mauaji na kufungwa, kisha akatoka kwa msamaha.

Pia, maeneo mengi ya fomu yake ilikosewa ikiwamo kutoweka sahihi fomu yake ya pingamizi.

Chanzo: mwananchi.co.tz