Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CCM yaonya kampeni za kuchafuana

CCM WEB CCM yaonya kampeni za kuchafuana

Fri, 30 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Sengerema, Mkoa wa Mwanza kimewaonya wagombea wanaochuana kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya CCM kufanya kampeni za kistaarabu bila kuchafuana ili kuepuka chuki na mpasuko baada ya uchaguzi kumalizika.

Rai hiyo imetolewa leo ijumaa Septemba 30 na Katibu wa CCM Wilaya ya Sengerema, Muhisin Zikatimu alipokuwa akizungumuza na waandishi wa habari ofisini kwake.

Amesema ndani ya uchaguzi lazima kutakuwa na makundi mbalimbali ya wagombea hivyo wagombea wasitumie nafasi hiyo kufanya kampeni za chuki ambazo siyo za kistaarabu zinazoweza kuleta mgawanyiko mkubwa ndani ya CCM.

Uchaguzi wa viongozi ndani ya CCM wilayani Sengerema unatarajia kufanyika Jumapili Oktoba 2 ambapo wanaCCM watakamilisha uchaguzi wa viongozi ndani ya wilaya.

Chaguzi za Jumuiya zilizofanyika wilayani Sengerema, Jane Msoga alichaguliwa kuwa mwenyeti wa UWT, Wilaya  Jacksoni Mazinzi alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi sambamba na Patric Mundeba aliyechaguliwa kuwa mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wilayani humo.

Makada wanaowania nafasi za Uenyeviti  wa CCM wilayani Sengerema ni Chasama Kamata, Daudi Masele sambamba Marco Makoye anayetetea nafasi yake.

Kwa upande wake Marco Makoye anayetetea nafasi ya uenyekiti  amesema yuko tayari kuendelea kuwatumikia wa CCM endapo wakimpatia tena ridhaa ya kuongoza nafasi hiyo.

Dr Omari Sukari anayewania nafasi ya ujumbe wa mkutano mkuu taifa, amesema wanaCCM   tunapaswa kuwa na umoja bila kubaguana ili tuisadie Serikali.

Amesema siasa za chuki hazina maana yoyote bali tuwashawishi wapigakura kwa hoja na sera nzuri ambazo zitatuweka salama.

Mmoja wanaCCM Juliana Charles amesema wanaCCM wataamua nani atakuwa mwenyekiti wa CCM ndani ya miaka mitano ijayo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live