Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CCM yamteua Shangai kugombe ubunge Ngorongoro

Ccmpicmm CCM yamteua Shangai kugombe ubunge Ngorongoro

Sun, 7 Nov 2021 Chanzo: mwananchidigital

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimemteua Emmanuel Shangai kuwa mgombea ubunge katika jimbo la Ngorongoro mkoani Arusha kwa tikeki ya chama hicho.

Shangai ameteuliwa kupeperusha bendera ya chama hicho kwenye uchaguzi mdogo baada ya kushinda katika uchaguzi wa kura za maoni katika jimbo hilo.

Uchaguzi huo mdogo utafanyika kutokana na kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo William Ole Nasha aliyefariki dunia Septemba 27, 2021 nyumbani kwake Jijini Dodoma.

Leo kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM imepitisha jina la Mwenyekiti huyo wa halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro kuwania uchaguzi huo unaotarajia kufanyika Desemba 11 mwaka huu.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shaka ametoa taarifa kwa vyombo vya habari kuwa, kikao cha uteuzi wa jina hilo kilifanyika Ikulu ya Chamwino chini ya Mwenyekiti wao Samia Suluhu Hassan ambapo kikao hicho kimepongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa kutimiza mwaka mmoja tangu kuchaguliwa kwake.

“Kamati Kuu imewateua Gulamhafeez Mukadam na Ella’s Masumbuko kugombea nafasi ya Meya wa Shinyanga Mjini,” inasomeka taarifa hiyo.

Tangu aliposhika nafasi ya kuwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia ameshaongoza vikao vya uteuzi kwa majimbo ya Ushetu, Konde, Buhingwe, Muhambwe na Ngorongoro ambako chaguzi zake zilitokana na vifo vya waliokuwa wabunge isipokuwa jimbo la Buhigwe mbunge wake Dk Philipo Mpango aliteuliwa kuwa Makamu wa Rais.

Chanzo: mwananchidigital