Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CCM yakutana kukamilisha uteuzi viongozi wa Wilaya

Samiaa Pic Ccm CCM yakutana kukamilisha uteuzi viongozi wa Wilaya

Mon, 26 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitafanya vikao vya kawaida vya uongozi ngazi ya Taifa Jijini Dodoma kuanzia leo Septemba 26, 2022 ambapo Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (CC) itaketi chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan.

Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa (NEC) itaketi Septemba 27 na 28 ambapo pamoja na mambo mengine vikao hivi vitakuwa na kazi ya kupokea mapendekezo, kujadili, kupitisha na kufanya uteuzi wa mwisho wa wanachama ambao wameomba uongozi katika ngazi ya wilaya.

Vikao hivyo vilitanguliwa na kikao cha Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Kilichofanyika tarehe 22 na 23 Septemba, 2022 Jijini Dodoma.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live