Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CCM yakanusha ukomo wa Urais wa Samia 2025

SHAKA SHAKA Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamidu Shaka

Wed, 11 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama cha Mapinduzi kimesikitishwa na upotoshwaji uliofanywa na gazeti la uhuru toleo number 24084 la leo jumatano, Lilochapisha habari kuhusu Rais Samia kutokuwa na Nia ya kuwania Urais 2025.

Katibu wa itikadi na uenezi CCM, ndugu Shaka Hamdu Shaka, amesema kuwa Gazeti hilo limepotosha sehemu ya mahojiano aliyofanya Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania na shirika la utangazaji La BBC Ikulu, kwa kuchukua sehemu ya mahojiano hayo tofauti na alivyoongea Rais Samia.

"Katika habari yake kuu imeandika kichwa cha habari kuwa "SINA WAZO KUWANIA URAIS 2025 - SAMIA" Huu ni upotoshwaji mkubwa wa kumlisha maneno Rais wa jamhuri ya muungao wa Tanzania Samia suluhu Hassan"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live