Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CCM yaibuka kidedea kata ya Turwa

11570 Turwa+pic

Mon, 13 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tarime. Chacha Mwita (CCM) amatangazwa ushindi katika uchaguzi wa udiwani kata ya Turwa mjini Tarime mkoani Mara.

Mwita amepata kura 1,401 na kufuatiwa na mgombea wa Chadema, Charles Mnanka aliyepata kura 1,121 huku Steven Chacha wa NCCR-Mageuzi akiambulia kura 17.

Leo jioni Jumapili Agosti 12, 2018 msimamizi msaidizi wa uchaguzi katika kata hiyo,  Peter Julius ametangaza matokeo hayo, kubainisha kuwa wapigakura walikuwa 2,539.

Kabla ya kutangazwa kwa matokeo  hao wafuasi wa Chadema walikuwa wakishangilia wakiamini kuwa mgombea wao ameshinda, baada ya kutangazwa matokeo hayo ikaelezwa kuwa aliyeshinda ni wa CCM.

Katibu wa Chadema Mkoa wa Mara,  Chacha Heche na mawakala wa Chadema wamesema matokeo hayo si halisi na kwamba mshindi ni mgombea wa Chadema.

Chanzo: mwananchi.co.tz