Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CCM yahamasisha wananchi kulipa kodi

18107 Pic+ccm TanzaniaWeb

Wed, 19 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Hai. Watanzania wametakiwa kuwa wazalendo kwa kulipa kodi kwa hiyari ili Serikali iweze kutekeleza miradi ya maendeleo na kuondoa changamoto zilizopo ikiwamo ubovu wa miundombinu.

Rai hiyo ilitolewa jana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kilimanjaro, Patrick Boisafi wakati akikagua miradi ya maendeleo wilayani Hai.

Alisema miradi ya maendeleo inayotekelezwa nchini fedha zinatokana na kodi za wananchi wenye nia njema na nchi yao

Alisema ni wajibu wa wananchi wanaopata kipato kinachozidi Sh4milioni kwa mwaka kuweka utaratibu wa kulipa kodi ili kuwezesha kupatikana kwa fedha za kutosha kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

“Tumetembelea miradi mingi ikiwamo huu wa skimu ya umwagiliaji wa Kikavu Chini lakini ni vyema watu wakatambua kuwa mambo haya yanafanyika kutokana na kodi zinazolipwa na wananchi,” alisema.

Boisafi aliwaonya watendaji wanaohujumu miradi ya Serikali kwa kufanya ubadhirifu na kusababisha itekelezwe chini ya kiwango.

“Serikali haina mchezo na mtu yeyote ambaye atafanya ubadhirifu na ndiyo maana sisi kama chama tumeelekezwa kufuatilia miradi hii ili kuona kama fedha zilizotolewa zimefanya yale yaliyokusudiwa.”

Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Kikavu Chini mbali na kuipongeza Serikali kwa jitihada za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo, pia waliomba kutafutiwa masoko ya uhakika waweze kuuza mazao yao.

Mwanaisha Selemani alisema Serikali imeboresha miundombinu ya umwagiliaji na kuwawezesha kulima mazao mbalimbali, lakini soko la uhakika ndio limekuwa tatizo.

Chanzo: mwananchi.co.tz