Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CCM yafuta kura za maoni, Dar yaongoza kwa rafu

81205 Ccm+pic CCM yafuta kura za maoni, Dar yaongoza kwa rafu

Tue, 22 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Katibu mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally ameagiza kurudiwa kwa uchaguzi wa wagombea uongozi wa serikali za mitaa ndani ya chama hicho katika maeneo yaliyolalamikiwa nchi nzima kwamba yamekiuka kanuni za uchaguzi huo.

CCM ilifanya uteuzi huo wa ndani ili kupata wagombea kwa ajili ya uchaguzi uliopangwa kufanyika Novemba 24.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ndogo za makao makuu ya chama hicho Lumumba jijini Dar es Salaam jana, Dk Bashiru pia ametaka mkoa wa Dar es Salaam urudie kazi hiyo ili kuhakiki mchakato wa uchaguzi.

“Yapo maeneo hawakufuata kanuni, na katika baadhi ya maeneo hayo kumekuwa na mgongano kiasi cha wanachama kususa kupiga kura,” alisema.

Kwa undani wa habari hii soma Gazeti la Mwananchi Oktoba 22, 2019.

Chanzo: mwananchi.co.tz