Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CCM yaanza mbio za ubunge

Shakaakakakakaka CCM yaanza mbio za ubunge

Fri, 29 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama Cha Mapinduzi kimewataka wanachama wake walio na nia na sifa ya kugombea ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki kujitokeza kuchukua fomu kuanzia Agosti mosi, 2022.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, amesema mchakato wa kuchukua na kurudisha fomu kupitia chama hicho utaanza Agosti Mosi hadi Agosti 10.

“Fomu hizo zitachukuliwa na kurejeshwa katika ofisi za CCM Makao Makuu Dodoma, Afisi Kuu ya CCM Zanzibar, na ofisi ndogo ya CCM Lumumba, Dar es Salaam, muda ni kuanzia saa mbili kamili asubuhi hadi saa 10 jioni, ”amesema Shaka.

Ametaja sifa za mtu anayestahili kugombea nafasi hizo kupitia CCM, ni awe ni mwanachama hai wa CCM, awe ni raia wa Tanzania, awe na sifa zinazo stahili kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Bunge la Tanzania, kwa mujibu wa masharti ya Ibara ya 67 ya Katiba ya Tanzania ya Mwaka 1977.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live