Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CCM yaanza kutoa fomu za makamu mwenyekiti

Ccmpicmm CCM yaanza kutoa fomu za makamu mwenyekiti

Sat, 25 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama cha Mapinduzi (CCM) wilayani Sengerema mkoa wa Mwanza, leo Jumamosi Juni 25, 2022 kimetangaza kuanza kutoa fomu za kugombea nafasi ya makamu mwenyekiti wa halmashauri za wilaya.

Uchaguzi wa nafasi hiyo utafanyika Julai 2022.

Katibu wa CCM wilaya ya Sengerema, Mhusini Zikatimu amesema hadi sasa Maxmiliani Mkugungu ambaye ni makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Buchosa amechukua fomu ya kutetea nafasi hiyo.

Amewataka madiwani wengine wajitokeze kuchukuwa fomu kutokana na chama hicho kuwa Demokrasia ya kweli ya kupata viongozi wake, ameeleza kesho Jumapili ni siku ya mwisho kuchukua fomu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live