Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CCM wapokea ripoti hali ya shule za jumuiya yake

29280 Pic+jumuiya+ccm TanzaniaWeb

Thu, 29 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Ripoti ya hali ya shule zilizo chini ya Jumuiya ya Wazazi ya CCM imependekeza mabadiliko ya muundo, mfumo wa uendeshaji na kiutendaji.

Ripoti hiyo imewasilishwa leo Novemba 28, 2018 na Mwenyekiti wa kamati iliyoundwa na Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM, Profesa Kitila Mkumbo.

Amesema umoja huo una shule 61 lakini kati ya hizo, shule 10 zimefungwa kutokana na kutokuwa na wanafunzi na kwamba zilizofanyiwa tathmini ni 51.

“Kwa ujumla shule za sekondari za wazazi zimetoa mchango mkubwa katika sekta ya elimu nchini na kwa muda mrefu ndio zimekuwa kimbilio kubwa la wazazi katika baadhi ya mikoa,” amesema.

Hata hivyo, amesema ili kufikia mzazi aamue kumpeleka mtoto wake katika shule za jumuiya ya wazazi wanapendekeza mabadiliko kwenye muundo, mfumo wa uendeshaji na kiutendaji.

Profesa Kitila amekataa kutoa ufafanuzi zaidi wa ripoti hiyo huku akieleza kuwa hawezi kuzungumzia kwa kina kilichomo ndani ya mapendekezo hayo kwa sababu chama bado hakijaimiliki ripoti hiyo.

Awali Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally amesema kamati hiyo inatokana na uamuzi uliotolewa na Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM kupata maoni ya kitaalamu.

Amesema maoni hayo yatawezesha kutekeleza mapendekezo ya uhakiki wa mali za CCM na jumuiya zake ambayo iliundwa na Halmashauri Kuu ya Taifa ikiongozwa na yeye, Profesa Kitila.

“Tunapokea tathmini na uchambuzi juu ya hali ya shule za wazazi na lengo likiwa ni kuhakikisha taarifa hiyo inatusaidia chama kuboresha mifumo na taratibu za kuendesha shule hizo ili nazo ziwe na mchango mkubwa katika kukuza maarifa,” amesema.



Chanzo: mwananchi.co.tz