Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CCM wampinga Spika Ndugai

Ccm Pic Data 1140x640.jpeg Job Ndugai, Spika wa Bunge la Tanzania

Sun, 2 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kilimanjaro, Patrick Boisafi amedai kuwa kauli aliyoitoa Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai, juu ya deni la taifa ni fedheha kwa Rais Samia Suluhu Hassan na uchochezi kwa nchi.

Boisafi ametoa amesema hayo wakati akitoa tamko la chama hicho kwa mkoa huo, ambapo amesema kiongozi huyo anapaswa kujitafakari

“Kauli aliyoitoa Ndugai ni fedheha kwa Rais Samia Suluhu Hassan, matamshi yale ni kama kejeli kwamba nchi inaweza kupigwa mnada, na ile ni kauli ya kichochezi ndani ya nchi yetu, kwa kuwa mama (Rias Samia Suluhu) ameitendea haki Serikali, kwani katika kipindi cha miezi tisa kila mtu ameshuhudia kilichofanyika na mambo mazuri yaliyoko mbele yanafurahisha” amesema Boisafi.

Boisafi amesema katika utaratibu mzima wa mkopo wa masharti nafuu wa Sh 1.3 trilioni, Bunge lilikaa wakaona ni namna gani fedha hizo zitumike kuleta maendeleo yatakayowagusa wananchi wote na baada ya hapo Rais aliita Halmashauri kuu ya chama hicho na viongozi wa mikoa kutoa muelekeo wa fedha hizo.

Itakumbwa hivi karibuni Spika Ndugai akiwa katika mkutano mkuu wa pili wa wanakikundi cha Mikalile Ye Wanyusi uliofanyika jijini Dodoma, alitetea uamuzi wa Bunge kuanzisha tozo za miamala ya simu, kuliko kuendelea kukopa.

“Juzi mama ameenda kukopa 1.3 trilioni. hivi ipi bora. Sisi Watanzania wa miaka 60 ya uhuru kuzidi kukopa na madeni au tubanane banane hapa hapa, tujenge wenyewe bila madeni haya makubwa makubwa yasiyoeleweka. Ni lini sisi tutafanya wenyewe ‘and how’ (na kwa vipi),” alisema Spika Ndugai.

“Tutembeze bakuli ndio heshima, tukishakopa tunapiga makofi, sisi wa kukopa kila siku,’ alisema Ndugai

“Tukasema pitisha tozo anayetaka asiye taka pitisha tozo, lazima tuanze kujenga wenyewe, nani atatufanyia, yuko wapi huyo mjomba, tukapitisha.

“Sasa 2025 mtaamua mkitoa waliopo nayo sawa waje watakaokuwa kazi yao kwenda kukopa, endapo hiyo namna ya ku-run nchi (kuongoza nchi) hivi sasa deni letu ‘seventy trilioni’ (Sh70 trilioni). hivi nyinyi si wasomi ‘is that healthy’ (hiyo ni afya). Kuna siku nchi itapigwa mnada hii,” alihoji Ndugai.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live