Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CCM wajipanga kuchukua Arusha Mjini

897c7dfdd18e0efc4183589c186c9592 CCM wajipanga kuchukua Arusha Mjini

Tue, 21 Jul 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WAJUMBE wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Arusha Mjini, wameaswa kuchagua watu sahihi kugombea ubunge, kwa kuwa jimbo linahitaji mtu anayekubalika kwa watu wote.

Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Kenani Kihongosi alisema hayo jijini Arusha jana kuwa huenda wagombea wamepitapita kwenye kata, lakini kura zitaamua nani atakayepata fursa ya kuchaguliwa.

Aliwaeleza wajumbe wa mkutano huo kuwa mgombea atakayechaguliwa na kama chama kitampitisha, anapaswa kuwa na uwezo wa kusimamia na kutetea maslahi ya wananchi wa jimbo hilo.

Katibu wa CCM Wilaya ya Arusha Mjini, Denis Mwita aliwaasa wajumbe kuhakikisha kuwa wanachagua mwanachama sahihi, atakayeuzika kwa wananchi na waache kuchagua kishabiki.

Mwita alisema mambo mengi yamekwama Arusha Mjini, kwa sababu hakuna mbunge kupitia CCM, hivyo aliomba wajumbe 487 wa mkutano huo kuhakikisha wanachagua watu sahihi Awali, mmoja wa wagombea waliochukua fomu, kuomba wapitishwe kugombea ubunge Arusha Mjini, Dk Clement Makere alijitoa kwa madai kwamba ametafakari kwa kina na kubaini kuwa endapo atachaguliwa, atashindwa kuwahudumia wagonjwa kwa kuwa taaluma yake ni daktari. Alisema hajaandaa mazingira rafiki ya kuwezesha wagonjwa wake, kupata huduma.

“Najitoa kwa sababu nina wagonjwa wengi na sijaandaa utaratibu wa kuwahudumia. Nikichaguliwa nitakuwa sijawatendea haki wagonjwa wangu, wacha niendelee kuwahudumia. Nawatakia wagombea wenzangu uchaguzi mwema”alisema Makere.

Chanzo: habarileo.co.tz