Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CCM kuvikutanisha vyama 38 vya dunia Dar

11400 Mkutano+pic%255C TanzaniaWeb

Sat, 14 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Chama cha Mapinduzi (CCM) kitakuwa mwenyeji wa mkutano wa kidunia utakaovikutanisha vyama 38 vya siasa kutoka Afrika.

Mkutano huo utakaofanyika Julai 17 hadi 18, 2018 utakuwa na washiriki 130 kutoka nje ya Afrika ni wa kwanza kufanyika Afrika, wa pili baada ya ule uliofanyika Beijing, China Desemba 2017.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Ijumaa Julai 13, 2018 na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole imesema mkutano huo umeandaliwa kwa ushirikiano wa CCM na Chama cha Kikomunisti cha China (CPC).

Baadhi ya watakaohudhuria mkutano huo ni Waziri wa Mambo ya Nje wa CPC,  Song Tao; Makamu wa Waziri wa Mambo ya Nje wa chama hicho, Xu Luping pamoja na Rais John Magufuli.

“Wazo la mkutano huu wa kidunia linatokana na fikra za Xi Jinping ambaye ni katibu mkuu wa CPC na Rais wa China,” inaeleza taarifa hiyo.

Inaeleza kuwa mada kuu ya mkutano huo ni vitendo na nadharia za vyama vya Afrika na CCP katika kufanya uchaguzi wa njia sahihi za kujiletea maendeleo na zinazoendana na mazingira ya Afrika.

“Pia kutakuwa na majadiliano ya kina na ya kweli, na kubadilisha taarifa na maarifa mbalimbali,” imesema taarifa hiyo.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz