Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CCM kumhoji Kangi Lugola

93814 Lugola Ccm+pic CCM kumhoji Kangi Lugola

Fri, 31 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Serengeti.  Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Mara kitamhoji aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania, Kangi Lugola baada ya kutuhumiwa kuhusika katika mkataba wenye harufu ya ufisadi uliosababisha Rais John Magufuli kutengua uteuzi wake.

Akizungumza na Mwananchi leo Alhamisi Januari 30, 2020 mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Mara, Samwel Kiboye maarufu ‘Namba Tatu’ amesema Lugola ambaye ni mbunge wa Mwibara atahojiwa na kamati ya maadili ya CCM mkoani humo.

“Tunayo sababu na mamlaka ya kumwita na kumhoji kwa sababu ni mbunge anayetokana na CCM na jimbo lake liko ndani ya Mkoa wa Mara.”

“Ni vikao vya CCM Mkoa wa Mara ndivyo vilivyomjadili na kupendekeza jina lake kwa ajili ya uteuzi kugombea nafasi ya ubunge uliompatia sifa ya kuteuliwa kuwa waziri,” amesema Kiboye.

Amesema Lugola kuhojiwa hakuhusiani na na taarifa ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ambayo itamhoji kesho Ijumaa Januari 31, 2020.

Kiboye amesema vitendo vinavyodaiwa kufanywa na Lugola vimemfedhehesha Rais Magufuli ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM.

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement
“Ataitwa lini, kikao kitafanyika wapi na tuhuma zipi tutamtaka ajibu linabaki kuwa suala la ndani ya chama. Ninachoweza kuthibitisha ni kweli tutamuita na kumhoji,” amesema Kiboye alipotakiwa kutaja ni lini mbunge huyo atahojiwa.

Chanzo: mwananchi.co.tz