Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CCM kukomboa majimbo yanayoshikiliwa na upinzani

5935 CCM .pngTZW

Fri, 6 Apr 2018 Chanzo: habarileo.co.tz

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja Tahir Ali amesema chama hicho kipo imara na kitahakikisha kinayakomboa majimbo yake yaliyochukuliwa na upinzani katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Alisema chama hicho kipo imara, kimejipanga vizuri kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 na kushinda kwa ushindi wa kishindo. Aliwataka viongozi ikiwemo wabunge na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuongeza mshikamano zaidi ambao utaleta ushindi na kuondokana na makundi. Aliutaja mshikamano huo ni pamoja na kutekeleza ilani ya uchaguzi kwa kuharakisha maendeleo pamoja na ahadi walizozitoa kwa wapiga kura.

Alisema huu sio wakati wa kupanga safu za uongozi kuelekea katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, kwani chama bado kinaendelea na utekelezaji wa ilani yake ya kuleta maendeleo kwa wananchi. “Wabunge na Wawakilishi wa jimbo la Kikwajuni na Jang’ombe wameonesha mshikamano ambao umewezesha kuzipatia ufumbuzi kero zinazowakabili wananchi,” alisema. CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kilipoteza majimbo mawili ya nafasi ya ubunge ambayo ni Mji Mkongwe pamoja na Mwanakwerekwe mjini Unguja.

Chanzo: habarileo.co.tz