Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CCM haina wasiwasi na Samia, atatekeleza yote

8699e91473aa843a380272485d350749.jpeg CCM haina wasiwasi na Samia, atatekeleza yote

Tue, 23 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Philip Mangulla amewahakikishia Watanzania wote kwamba pamoja na Taifa kuondokewa Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli mambo yanataenda kama yalivyopangwa chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza wakati wa Mazishi Rasmi ya Kitaifa ya Dk Magufuli katika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma jana, Mangulla alisema ni kweli Tanzania imepoteza Rais Magufuli ambaye alizoeleka na tulikuwa naye.

Alisema Watanzania wanatakiwa kuondoa wasiwasi kwani viongozi hao wawili, Dk Magufuli na Rais Samia walizunguka nchi nzima wakiinadi Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2015 na ile ya mwaka jana, 2020-2025, hivyo Rais Samia anajua mipango yote ya chama na serikali.

“Mambo yote yataenda kama yalivyokuwa yamepangwa, niwatoe wasiwasi Watanzania mambo yataenda vizuri kwani walikuwa wakizunguka nchi nzima wakipeperusha bendera ya CCM na kunadi ilani ya chama, mambo yataenda vizuri,” alisema mwanasiasa huyo mkongwe.

Mangulla alisema Samia ana uzoefu wa kutosha kutokana na ukweli kwamba kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2015, alizunguka nchi nzima pamoja na Dk Magufuli katika nchi nzima akidadi Ilani ya Uchaguzi.

Alisema hata kabla ya uchaguzi wa mwaka jana, Samia alizunguka tena pamoja na Dk Magufuli wakiinadai Ilani ya Uchaguzi Mkuu yenye ukurasa 303, hivyo anajua ni kitu gani kipo kinachotakiwa kutekelezwa katika ilani hiyo.

Alisisitiza anajua nini kipo kwenye Ilani ya Uchaguzi cha kutekeleza katika kipindi cha miaka mitano ijayo hadi 2025 hasa baada ya Watanzania takribani asilimia 84.7 kuukubali uongozi wa chama baada ya Dk Magufuli na Rais Samia kufanya vizuri na katika tathmini ikaonesha wamefanya vizuri na kuchaguliwa kuongoza tena nchi.

Alisema serikali imeweka mipango ya namna ya kutekeleza maekelezo yaliyopo kwenye ilani kupitia Mpango ya Maendeleo wa Miaka Mitano ambao unatakiwa kujadiliwa bungeni na kupitishwa.

Alisema kutokana na viongozi hao wawili kuzunguka nchi nzima kunadi Ilani ya CCM, Watanzania wasikate tamaa kwamba Dk Magufuli ameondoka sasa mambo yatakuwaje wakati Samia anajua nini kinatakiwa na yataenda vizuri.

Alisema ameteta na Spika wa Bunge, Job Ndugai akiuliza ni lini Bunge litajadili na kupitia Mpango wa Serikali wa Miaka Mitano, akasema Spika amesema utajadiliwa katika Bunge la Bajeti linaloanza Machi 30, mwaka huu.

Alisema Samia atatekeleza mipango hiyo ya maendeleo ambayo tayari imeandaliwa na Bunge litapisha kwa ajili ya utekeleza wake kwa miaka mitano 2020/21-2025/26.

Chanzo: www.habarileo.co.tz