Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CCM Zanzibar yawaapisha wanaume kuacha ukatili

CCM WEB CCM Zanzibar yawaapisha wanaume kuacha ukatili

Tue, 7 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamu wa pili wa Rais amewaapisha baadhi ya wanaume katika ziara yake mkoani Tanga, kiapo cha kutofanya ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika vitendo vya ubakaji na ulawiti kwa madai kuwa suala hili linachafua taswira njema ya nchi yetu ambayo ni kisiwa cha amani na utulivu.

Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Seleiman Abdulla ameyasema hayo wakati wa maadhimisho ya ziara yake ya siku 6 mkoani Tanga, kwenye ukumbi wa Liger Naivera jijini Tanga kwa kuwaasa wanaume kuacha ukatili dhidi ya watoto na wanawake kwa kusisitiza kuwa nchi yetu tunapata aibu, tunapata kashfa, tunapata fedheha kutokana na udhalilishaji wanawake na watoto ambao unafanywa na Wanaume, Hali iliyopelekea kuwapisha baadhi ya wanaume walihudhulia siku hiyo.

Mambo mengine aliyokazia ni pamoja na viongozi kusimamia haki katika utatuzi wa migogoro, kukaribisha wawekezaji, utunzaji wa mazingira na ujio wa meli ya kibiashara bandari ya Tanga ambayo itachochea kasi ya ukuaji wa uchumi wa mkoa huu, Hata hivyo makamu wa pili wa Rais amekiri kufurahia ziara yake mkoani Tanga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live