Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CCM Yazindua Kadi Mpya za Kielektroniki

Ccm Kadi CCM Yazindua Kadi Mpya za Kielektroniki

Sat, 5 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimezindua kadi mpya za wanachama za kielektroniki zenye taarifa na kumbukumbu muhimu za mwanachama zitakazowatambulisha na kuwawezesha kupata huduma za kifedha.

Uzinduzi wa kadi hizo umefanyika mjini Musoma leo Jumamosi Februari 5 ikiwa ni sehemu ya kilele cha maadhimisho ya miaka 45 ya kuzaliwa kwa chama hicho tawala kilichoundwa Februari 5, 1977 baada ya kuungana kwa vyama vya ukombozi vya Tanganyika African National Union (TANU) na Afro Shirazi Party (ASP) kwa upande wa Zanzibar.

Kadi hizo zimezinduliwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Samia Suluhu ambaye pia amekabidhiwa kadi ya kwanza na Katibu Mkuu wa chama hicho, Daniel Chongolo.

Akizungumza muda mfupi kabla ya kuzinduliwa kwa kadi hizo Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo amesema kupitia kadi hizo wanachama wa CCM zaidi ya milioni 12 siyo tu watatambulika kirahisi, bali pia wataweza kutumia kadi zao kupata huduma za kifedha.

Chongolo, amesema wanachama zaidi ya milioni 2.7 tayari wamesajiliwa kupitia mfumo huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live