Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CCM YATOA MAAGIZO AJIRA, HUDUMA ZA UCHUMI

8508804a95bd82309c2c77c5841df2f1 CCM YATOA MAAGIZO AJIRA, HUDUMA ZA UCHUMI

Fri, 25 Jun 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kinaridhishwa na jitihada za serikali katika uwekezaji ikiwa ni pamoja na kujenga mazingira mazuri ya kuaminika na kuvutia wawekezaji nchini.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka alisema hayo wakati akizungumza na ujumbe wa watendaji wa ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji uliongozwa na Profesa Godius Kahyarara.

Shaka alisema CCM inaitaka serikali iendelee kutengeneza fursa za ajira, kukuza uchumi na kuongeza pato la taifa kupitia uchumi wa viwanda kama ilivyoelekezwa katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020- 2025.

“Chama Cha Mapinduzi kinaielekeza Wizara kuendelea kutekeleza mambo yaliyoainishwa katika Ibara 17, 18, 22 mpaka 32 ambapo kwa mwaka 2020 mmeanza vyema kwa kuanza kusajili miradi 169 iliyozalisha ajira 10,000 na kufikia Aprili 2021 miradi 150 imesajiliwa ambapo kiwango cha ajira hakijafikia lengo hapa tuna kazi ya kufanya na maelekezo ya Chama mkajipange vyema,” alisema.

Shaka alisema CCM pia inaitaka wizara hiyo iendelee kuhamasisha sekta binafsi kutumia sayansi, teknologia na ubunifu ili kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji kuwekeza hasa katika kufanya utafiti wa teknologia za kisasa.

“Shirikianeni na Wizara ya Fedha kuimarisha huduma za kiuchumi, kifedha na upatikanaji wa mikopo. Lazima muweke mkazo zaidi katika kuwalinda, kuwasimamia wawekezaji walioko chini ili waendelee kukua na kuimarika zaidi na waone nchi yetu ndio sehemu sahihi ya uwekezaji duniani” alisema.

Profesa Kahyarara alisema wizara imepiga hatua katika kuandaa mazingira ya uwekezaji na kukamilisha maandalizi ya kuanza kwa kongano za viwanda hasa katika maeneo ya ya Kibaha, Magu, Manyoni, Kilosa na Mufindi kwenye awamu ya kwanza.

“Hali ya uwekezaji nchini sio mbaya tumepiga hatua kubwa muda sio mrefu tutawajuilisha watanzania namna serikali ya Rais Samia ilivyofanikiwa kwa kiasi kikubwa katika eneo hilo, aidha miradi mikubwa miwili ipo mwishoni kuanza uchakataji wa alizeti na uzalishaji wa sukari ambayo itazalisha ajira 325,000 ambazo zitakuwa ni sehemu ya ukombozi mkubwa kwa vijana,”alisema.

Chanzo: www.habarileo.co.tz