Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CCM YATANGAZA MAOMBOLEZO SIKU 21

JPM CCM4 CCM YATANGAZA MAOMBOLEZO SIKU 21

Fri, 19 Mar 2021 Chanzo: zanzibar24.co.tz

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole, ametangaza siku 21 za maombolezo kufuatia kifo cha Mwenyekiti wa chama hicho na aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli.

Hayo ameyasema wakati akitoa tamko la chama kufuatia kifo cha Mwenyekiti wao na kusema kuwa Halmashauri Kuu ya chama hicho itaketi Jumamosi ya Machi 20.

“Wakuu wa chama waliopo Mzee Phillip Mangula Makamu wa Mwenyekiti Tanzania Bara na Mzee Ali Mohamed Shein Makamu wa Mwenyekiti Zanzibar wameshauriana na kukubaliana kwamba Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa iketi kwa kikao maalum Jumamosi ya Machi 20 saa 8:00 mchana,” amesema Polepole.

Aidha Polepole ameongeza kuwa “Aidha taarifa inatolewa kwamba chama kitakuwa kwenye maombolezo ya siku 21 sambamba na tangazo la Serikali, wakati wote huo bendera za Chama Cha Mapinduzi zitapepea nusu mlingoti”.

Mbali na hayo chama hicho pia kimetoa rai kwa Watanzania kuendelea kuwa watulivu, “Uongozi wa chama unawaomba wanachama wote wa CCM, watu wote wenye mapenzi mema ya nchi yetu, Watanzania wote kwa ujumla kuwa na moyo mkuu, kuendelea kuwa watulivu, kusimama imara na kuendelea kutafakari mchango wa kipekee wa ndugu yetu John Pombe Magufuli,” ameongeza Polepole.

Chanzo: zanzibar24.co.tz