Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CCM Urambo wana imani na Rais Samia

19b87a6a82bf815ffd5784b7bb4e0687.png CCM Urambo wana imani na Rais Samia

Wed, 31 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

WANANCHI na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Urambo mkoani Tabora wamesema wanaimani na serikali ya awamu ya tano itaenda kukamilisha miradi ya maendeleo iliyoachwa na Dk John Magufuli.

Katika kipindi cha miaka 5 iliyopita ndani ya uongozi wa Dk John Magufuli serikali ilitekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ya sekta ya elimu, ujenzi wa vituo vya afya viwili ,maji kutoka Ziwa Victoria, miundombinu ya barabara kwa kiwango cha lami na kituo cha kupozea umeme.

Katibu wa siasa na uenezi wa wilaya ya Urambo, Obed Balola alisema wanaimani Mama Samia Suluhu Hassan ataenda kukamilisha miradi hiyo

Katibu wa Umoja wa Vijana na Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wilayani Urambo, Mubaraka Kasendeka alisema wanamuombea Mungu afya na amani ili aweze kuwatumikia wananchi.

"Tunamuombea afya huyu mama aongoze taifa letu na kama wananchi tutazidi kumuombea hekima na amani pia maamuzi yake yawe na msimamo kuwasidia wananchi wake"alisema katibu huyo.

Chanzo: www.habarileo.co.tz