Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CCM Singida wapigana marufuku

Kilimbah Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Juma Killimbah

Mon, 7 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Alhajj Juma Killimbah amesema kiongozi yeyote wa chama hicho hana mamlaka ya kumfukuza mtu yeyote uanacha.

Killimbah ambaye alikuwa mgeni rasmi aliyasema hayo juzi wakati akihutubia katika maadhimisho ya sherehe za kuzaliwa kwa CCM miaka 45 kwa mwaka 2022 Wilaya ya Singida Mjini.

"Mnapata wapi mamlaka ya kuwafukuza watu uanachama mwenye mamlaka ya kumfukuza mtu uanachama ni kikao pekee cha mkoa ambacho mwenyekiti wake ni mimi na sio vinginevyo ebu hayo matatizo yenu madogo madogo yamalizeni" alisema Killimbah.

Alisema kama kunakiongozi atakuwa amekosea wanaweza kumfukuza lakini sio mwanachama kwani ambaye anafukuzwa kwa taratibu zilizopo zikiwemo za kumuonya zaidi ya mara moja kwa kupitia kamati za maadili.

Akizungumzia mafanikio waliyopata katika kipindi cha miaka 45 tangu kuzaliwa kwa chama hicho alisema kila wilaya imefanikiwa kujenga ofisi za kisasa za chama hicho huku akizitaja kuwa ni Mkalama, Iramba, Ikungi, Manyoni, Itigi, Singida Vijijini huku wilaya ya Manispaa wakiendelea na mchakato wa ujenzi.

Killimbah alitumia nafasi hiyo kuwaomba Wana CCM wenye sifa kujitokeza kugombea nafasi ya uongozi kwenye uchaguzi wa ndani wa chama hicho utakaofanyika kuanzia Aprili 14 mwaka huu kwa kuanzia na vitongoji.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Singida Mjini, Lusia Mwiru alisema changamoto kubwa iliyopo ni wanachama wengi kwa zaidi ya miaka miwili wamepigwa picha ili waweze kuingizwa kwenye mfumo wa kielekritoni baada ya kufanya taraibu zote lakini hadi leo hii hawajapata kadi zao jambo ambalo linawavunja nguvu hivyo aliomba suala hilo lishughulikiwe haraka.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (MNEC) Mkoa wa Singida Yohana Msita alisema katika kipindi hiki cha miaka 45 ya CCM nchi chini ya chama hicho imefanya mambo mengimakubwa ya maendeleo.

Alisema suala la kuongoza nchi sio la rahisi kama watu wengine wanavyo lifikiria na kuwa CCM ni Baba na Mama kwani kimetutoa mbali hivyo kila mtu anastahili kukipongeza.

Msita alitumia nafasi hiyo kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan na watangulizi wake kwa kusimamia vizuri ilani ya chama kwa kusimamia nchi katika nyanja mbalimbali na kujenga imani kwa wananchi ya kuendelea kushika dola.

Katibu wa CCM Mkoa wa Singida Lucy Boniphace alisema miongozo iliyoweka wakati wa maadhimisho hayo ni viongozi kuhamasisha wananchi kulipa kodi zikiwemo za majengo.

Katika maadhimisho hayo baadhi ya mambo yaliyofanyika ni kutembelea na kujionea eneo la ujenzi wa ukumbi na Ofisi ya CCM Wilaya, mada mbalimbali zilitolewa ikiwepo ya maadili ya viongozi, Mada ya Uzalendo iliyotolewa na Mbunge wa Singida Mjini Mussa Sima na maelezo mafupi ya maadhimisho ya sherehe za kuzaliwa kwa CCM miaka 45 kimkoa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live