Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CCM Shinyanga yatishia kufuta waomba ubunge

93d2a1566cd85275b9b2c1a596b2d333.png CCM Shinyanga yatishia kufuta waomba ubunge

Sun, 19 Jul 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

CHAMA cha Mapinduzi ( CCM) mkoani Shinyanga kimetishia kuwafuta wanachama wake wote wanaotaka kuwania jimbo la Shinyanga Mjini kwa tiketi yake kutokana na baadhi yao kuwatembelea majumbani wapiga kura ndani ya chama na kuonesha dalili za kutoa rushwa.

Idadi kubwa ya watia nia ni vijana na robo tatu wanaelimu ya Shahada na wapiga kura za maoni ndani ya chama ni 449.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Katibu wa CCM mkoa wa Shinyanga, Donald Magesa alipokuwa katika kikao cha dharura na waombaji 60 wa jimbo la Shinyanga mjini na kuwaeleza kuwa mienendo ya wengi wao imekuwa siyo mizuri .

Magesa alisema kuwa chama cha Mapinduzi kinataka kiongozi aliye halali sio kwa njia ya kutoa fedha kwani kupata kura nyingi siyo kigezo cha kukuchagua hasa kama hufuati taratibu za chama na kanuni zake ikiwemo maadili.

“Nimekuja na maneno makali leo kutokana na baadhi yenu kunichefua kwani wameonekana kushiriki katika vitendo vya rushwa kwa kuwazungukiwa wajumbe nyakati za usiku majumbani mwao nakuwaomba wawapigie kura,” alisema Katibu Magesa.

Alisema katika mkoa wa Shinyanga waliochukua fomu ni 324 na mmoja ndio hajarudisha kutoka jimbo la Ushetu, Kishapu waliochukua fomu na kurudisha ni 78, Shinyanga Mjini 60, Solwa ni 54, Kahama mji 70, Msalala ni 44 na Ushetu ni 18.

Aidha kati ya waliochukua fomu 324 wanaume ni 298 na wanawake ni 26, Msalala ni wanawake wawili, Solwa wanne, Kahama mji nane, Kahama mji saba na Ushetu ni mmoja.

Chanzo: habarileo.co.tz