Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CCM: Rais Samia ameupiga mwingi

CCM 10.jpeg Rais Samia

Fri, 18 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo amesema Chama hicho kinaridhishwa na utekelezaji wa Ilani ya CCM na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu ambaye ndiye Mwenyekiti wa CCM Taifa kwa utekelezaji huo wa Ilani kwa kasi.

Chongolo amesema hayo leo Ijumaa, Machi 18, 2022 wakati akizungumza na wanahabari.

“Ndani ya mwaka 1 kumekuwa na mafanikio na mapinduzi makubwa. Kwa mara ya kwanza wanafunzi wa kidato cha kwanza wameanza shule kwa pamoja bila kuwepo wanaosubiria nyumbani baada ya ujenzi wa madarasa 12,000 na 3000 ya shule shikizi ndani ya miezi mitatu pekee.

"Tanzania kwa kipindi cha mwaka mmoja kimeendelea kujiimarisha zaidi Kiuchumi, Kijamii na Kisiasa na ulinzi wa mipaka ya Tanzania upo imara pamoja nankuimarisha Muungano.

"Ziara za Rais Samia Samia zimekuwa na..anufaa makubwa sana.kwa Diplomasia ya Uchumi na kudumisha Amani Kikanda na Kimataifa huku Tanzania ikiwa mstari wa mbele khimarisha Amani, Utawala Bora na Haki za Binadamu.

"Miradi ya kimkakati ya kuzalisha Umeme inaendelea kutekelezwa na hiyo imeondoa adha ya umeme kwa Wananchi na tayari mikoa yote imeunganishwa na Gridi ya Taifa isipokuwa mikoa minne tu ya Kagera, Kigoma, Katavi na Rukwa ambayo pia itaunganishwa.

"Ujenzi wa Reli ya kisasa Standard Gauge unaendelea vizuri na Mhe. Rais

Samia ameahidi kuwa ujenzi wa reli hiyo utakamilika na tayari yanafanyika mazungumzo na nchi jirani itakakofika reli hiyo na kufungua Uchumi, hakika kazi inaendelea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live