Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CCM Masasi wamlilia Hayati Magufuli

CCM00 1?fit=640%2C402 CCM Masasi wamlilia Hayati Magufuli

Wed, 24 Mar 2021 Chanzo: ippmedia.com

Miongoni mwa miradi hiyo ambayo imefanywa na Hayati Magufuli ni pamoja na ujenzi wa shule ya msingi ya Kisasa Kitunda, vituo vya afya, zahanati, madarasa, maji, umeme na miundombinu ya barabara.

Hayo yalisemwa leo Mjini Masasi na Mwenyekiti wa chama hicho, wilaya ya Masasi, Edward Mmavele, alipokuwa akitoa salamu za maombolezo kwa wanachama ambao walikusanyika katika ofisi za CCM Masasi kwa ajili ya kuomboleza msiba huo.

Amesema Chama cha Mapinduzi wilaya ya Masasi na wananchi kwa ujumla wameumizwa na kusikitishwa na kifo cha Rais Dk. Magufuli kwa sababu ameondoka wakati bado Wanamasasi walitamani kuendelea kumuona akiwafanyia mambo makubwa zaidi ya kimaendeleo, hivyo kufuatia kifo chake ni wazi kuwa taifa limepoteza kiongozi mpambanaji na shujaa wa wananchi wanyonge ambao ni masikini.

Mmavele amesema Hayati Rais Dk. Magufuli ni nuru ya Afrika iliyozimika ghafla hivyo wana CCM na wananchi wa wilaya ya Masasi kamwe hawatasahau mazuri yote ya kimaendeleo yaliyofanyika chini ya serikali yake akiwa madarakani kabla ya umauti wake.

Chanzo: ippmedia.com