Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CCM KUZINDUA KAMPENI RASMI ZANZIBAR SEPTEMBA 12

Capture 382?fit=764%2C653 CCM KUZINDUA KAMPENI RASMI ZANZIBAR SEPTEMBA 12

Thu, 10 Sep 2020 Chanzo: zanzibar24.co.tz

Chama cha Mapinduzi – CCM kimewataka wanachama wake wote na wananchi kwa ujumla kudumisha amani na utulivu katika kipindi hichi cha kampeni na kuelekea uchaguzi mkuu.

Hayo yameelezwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdalla Juma Saadala (Mabodi) wakati akizungumza na waandishi wa habari huko afisi kuu za chama hicho Kisiwandui Mjini Zanzibar.

Amesema Chama cha Mapinduzi kinatarajia kuzindua kampeni zake rasmi Jumamosi Septemba 12 katika viwanja vya Demokrasia kibandamaiti ambapo mgombea wa Urais wa Zanzibar Dk. Hussein Mwinyi atanadi sera zake.

Aidha Dk. Mabodi amewataka wananchi wote wa Zanzibar kujitokeza kwa wingi viwanjani hapo kusikiliza sera za Chama cha Mapinduzi ambazo zitasindikizwa na wasanii mbalimbli watakaokuwepo kwaajili ya kutumbuiza.

Sambamba na hayo Dk. Mabodi amepinga vikali kauli zinazotolewa na baadhi ya watu wanaokirushia lawama Chama cha Mapinzuzi kuwa hakifati sheria na kinahatarisha amani kwa kutumia vyombo vya dola jambo ambalo sio kweli.

Chanzo: zanzibar24.co.tz