Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CCM Ileje yafurahishwa na utekelezaji wa Ilani ya chama

Dds.png Wajumbe wa Halmashauri kuu ya Ccm Ileje wakipata mrejesho

Tue, 1 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wajumbe wa mkutano wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ileje mkoani Songwe wameridhishwa na namna viongozi wa Halmashauri ya Ileje wanavyotekeleza Ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025 wilayani humo .

Wajumbe hao wamesema hayo wakati wa mkutano wa halmashauri kuu ya chama hicho wilayani humo ambao umefayika Februari 28 mwaka huu katika ukumbi wa Chama cha Mapinduzi(CCM) uliopo Itumba, kwa kuongozwa na mwenyekiti wake Hebron Kibona ambapo pamoja na mambo mengine, Mkutano huo umepokea na kujadili taarifa za utekelezaji wa Ilani ya CCM kuanzi mwezi Julai hadi Disemba mwaka 2021 kutoka katika wilaya hiyo, na baadhi ya taasisi ikiwepo TANESCO, TARURA, RUWASA,na Idara ya Afya na Elimu.

Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM, mkuu wa wilaya ya Ileje Anna Gidarya amesema katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021/2022 kwa kipindi cha mwezi Julai hadi Desemba wilaya ya Ileje imepokea fedha mbali mbali za miradi ya maendeleo katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi na kufanikisha kuzisimamia kama maelekezo yalivyotolewa.

Gidarya amesema katika sekta ya afya walipokea fedha za kukamilisha ujenzi wa maboma katika zahanati za vijiji vya Ilanga ,Igoje na Chembe ambapo jumla ya shilingi milioni mia moja hamsini (150) zilitolewa na kila zahanati kutengewa shilingi milioni hamsini ( 50) sambamba na fedha shilingi milioni miatano (500) kwa ajili ya ujenzi wa wodi 3 za wagonjwa katika hospitali ya wilaya iliyopo Itumba

Gidarya amesema pia serikali imetoa fedha shilingi milioni 250 zilizotokana na tozo ya miamala kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya Ndola ambapo shughuli ya ujenzi inaendelea , pia zaidi ya fedha shilingi milioni mia sita ( 600) za Uviko zilipelekwa katika halmashauri ya Ileje kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa zaidi ya 30 vya shule za msingi na sekondari .

Aidha Gidarya imewapongeza mamlaka ya maji wilaya Ileje RUWASA chini ya usimamizi wa meneja wa mamlaka hiyo Mhandisi Endrw Tesha, kwa kushika nafasi ya kwanza Kitaifa baada ya tathimini kufanyika na kubaini wanaongoza kwa kila mwaka kuongeza vituo vya maji vijijini na kuzitaka idara zote kuiga utendaji na uwajibikaji kuzingatia Ilani ya chama cha mapinduzi.

Mwenyekiti wa chama wilayani humo Hebron Kibona fedha za miradi zinazopelekwa na serikali wilayani humo zinapaswa kusimamiwa ili wananchi waendelee kuneemeka na matunda na mafanikio ya serikali ya awmu ya sita ikiongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Kwa upande wake Katibu wa chama wilayani humo Hassan Lyamba amesema katika kutekeleza mipango ya serikali , ni wajibu wa wenyeviti na makatibu kata wa chama hicho kusimamia ajenda ya mapato ili kuongeza wigo wa ukusanyaji mapato.

Lyamba amesema usomaji wa taarifa hiyo kumeenda sambamba na uzinduzi wa ugawaji wa kadi za wananchama za kielektroni kwani jumla ya wanachama 256 wanatarajia kugawiwa kwa awamu ya kwanza, ambapo kata ya Chitete wanachama 222 , Ikinga 23, Bupigu 18, Itumba 2 na Mlale 1.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live