Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CCM Haina Ukanda, CCM si Mali ya Serikali

Kinana Ccm.png Abdulrahman Kinana

Fri, 1 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Mkuu wa zamani wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana amechaguliwa na Wajumbe wa Mkutano Mkuu leo kuwa Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara wa Chama hicho, Kinana amepata kura zote 1,875 zilizopigwa sawasawa na ushindi wa 100%.

Wajumbe 1,875 wamehudhuria Mkutano Mkuu wa CCM unaofanyika leo tarehe Mosi Aprili 2022 jijini Dodoma, sawa na asilimia 99.2 ya wajumbe wote 1,889 ambapo ni wajumbe 14 waliokosa kwa dharura.

Akitoa neno la shukrani baada ya kuchaguliwa, Kinana amesema; “Baada ya shukrani niseme yafuatayo kazi yng ya kwanza ningependa kukuhakikishia ni kukuimarisha Chama, kiwe imara kiheshimike na watanzania na ili kiwe imara, lazima demokrasia iwe imara na ili kiwe imara lazima tusimamie haki.

“Tukiweza kuimarisha haki ndani ya CCM tutaimarisha nje ya CCM, tumemfuatilia mara kadhaa Mwenyekiti hata juzi akipokea tipoti ya CAG nilimsikia akisema vyeti peke yake si sifa. Vyeti viende na sifa, vyeti viende na uadilifu, vyeti viende na uhodari.

“Lazima tusimamie haki, nchi hii inajulikana Kwa haki ukienda nje watanzania tunajulikana kwa haki. Lazima tuwe mfano wa kusimamia na kutetea haki na kukataa dhulma.

"CCM si mali ya serikali ila serikali hizi zinatoka CCM, CCM hatupokei maelekezo kutoka serikalini, Serikali haiiagizi CCM bali CCM inaiagiza serikali kupitia ilani zake, na wanaoenda kuomba kura ni CCM na si Serikali” Kinana.

"Chama hichi (CCM) kikubwa, penda usipende Chama hichi kinapendwa na Watanzania, Chama hichi ni masikio ya Watanzania lazima tujenge utamaduni wa kuwasikiliza na kutatua matatizo yao lazima tuwajali na watatuchagua tu.

“Hichi Chama (CCM) kina watu wengi sana lakini kuna watu wanakipenda sana lakini si wanachama, ndaki ya hiki Chama hakuna ukanda, ukabila, Udini, mtu akikosa hoja anaingia kwenye kichaka cha ubara Na ukabila si Sawa

“Mh. Rais nikushukuru sana kwa imani yako kwangu, nikushukuru sana kwa matumaini yako kwangu, nikushukuru sana kwa matarajio yako kwangu…juzi uliniita ukaniomba niwe Makamu Mwenyekiti, nikasema sina hiana nimekubali, nikuahidi kwa kifupi sitakuangusha.

“Kazi yangu ya kwanza ni kuimarisha chama kiwe chama imara kinachoheshimika na ili kiwe imara lazima demokrasia iwe imara na ili demokrasia iwe imara lazima kusimamia haki. Haki ya kuchaguliwa na haki ya kuchagua bila upendeleo, bila mizengwe, bila rushwa, bila umaarufu.

“Haki ya pili ni haki ya kutoa mawazo lazima wanachama wawe huru kutoa mawazo hakuna mwenyehaki miliki ya mawazo, lazima tusikilize kila mwanachama ili tuweze kumsikiliza kila mwananchi. Si sawa mwana CCM kwenda hadharani kuisema serikali yake vibaya,” amesema Mzee Kinana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live