Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CCM, CPV wateta, waahidi ushirikiano

Chongolo New Daniel Chongolo, Katibu Mkuu CCM

Tue, 20 Sep 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

 Chongolo amesisitiza hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Makamu Mwenyekiti wa Mambo ya Nje wa CPV, Troung Quang Hoai Nam jana Jumatatu Septemba 19, 2022 katika Ofisi ndogo za Makao Makuu ya CCM, Lumumba, jijini Dar es salaam.

Ameeleza umuhimu wa kuboresha na kuimarisha mahusiano yaliyopo kati ya vyama hivyo ambayo yanalenga kupanua wigo wa ushirikiano katika maeneo mbalimbali yakiwapo uwekezaji katika kilimo, biashara na mafunzo na kubadilishana uzoefu wa kiuongozi kwa viongozi na wanachama wa vyama vyote viwili.

Katika mazungumzo hayo, Chongolo amesisitiza namna ambavyo Tanzania imeweka mkazo katika kilimo cha umwagiliaji kuwa mojawapo ya mikakati ya kukabili na kupunguza tatizo la ajira kwa vijana.

Amesema ushirikiano katika eneo hilo utatengeneza fursa za kuajiri watu wengi huku akibainisha kuwa Serikali fedha nyingi katika eneo hilo ili kuvutia uwekezaji, kuongeza uzalishaji wenye tija na kukuza uchumi.

Kwa upande wake Troung pamoja na mambo mengine kwa niaba ya CPV ametilia mkazo wa kudumisha, kukuza na kuendeleza zaidi ushirikiano katika kuzalisha ajira kupitia uwekezaji katika Sekta ya Kilimo cha umwagiliaji.

Amesema Vietnam imefanikiwa sana katika kilimo hicho kutokana na kuwa na miundombinu iliyojengwa miaka ya nyuma.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz