Chama Cha Mapinduzi (CCM), kinawashukuru Watanzania kwa kuendelea kukiamini na kukipatia ushindi wa kishindo katika uchaguzi mdogo uliofanyika 17 Desemba, 2022 kujaza nafasi ya Ubunge Jimbo la Amani wilaya ya Mjini mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar pamoja na udiwani uliofanyika katika kata 7 kati ya 12 ambazo ni Majohe (Dar es Salaam), Mwamalili (Shinyanga) Njombe (Njombe), Vibaoni, Mnyanjani (Tanga), Mndubwe (Mtwara), Dunda (Pwani) na Kata 5 kati ya 12 tayari Chama Cha Mapinduzi kilishinda kwa kupita bila kupingwa, kata hizo ni Dabalo (Dodoma), Ibanda (Mbeya), Misugusugu (Pwani), Kalumbeleza (Rukwa) na lukozi (Tanga).
Siri ya ushindi huu wa CCM ni umoja na mshikamano uliopo ndani ya chama, uteuzi wa wagombea bora, kampeni za kisasa zilizowafikia wapigakura, uadilifu na uaminifu katika kuwatumikia wananchi hususani katika kukidhi mahitaji na matarajio yao katika kuwaletea maendeleo. Kazi ambayo inafanywa kwa weledi na ustadi mkubwa na serikali zake zikiongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na Dkt Husein Ali Mwinyi kupitia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025.
Kushindwa kwa vyama vya upinzani ni muendelezo wa ushahidi kwamba havikubaliki na Watanzania wameendelea kuwathibitishia kwamba hawajazoea siasa za vurugu, ulaghai, ubinafsi na migawanyiko ambazo hazina tija katika ustawi wa maisha na maendeleo yao.
CCM inaahidi kuendelea kuwatumikia Watanzania kwa amani na utulivu kwa kuwa ina uzoefu wa kufanya siasa za kistaarabu na maendeleo kwa ustawi wa watanzania wote. Ndio maana imeendelea kukubalika kwa wananchi.
Taarifa hiyo imetolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shaka.