Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bwege: "Mwanasiasa Haogopi Kufungwa Wala Kufa, Naunga Mkono Tozo"

Bwege?fit=848%2C469&ssl=1 Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Kilwa Kusini, Suleiman Bungara (Bwege)

Thu, 5 Aug 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Kilwa Kusini, Suleiman Bungara maarufu kwa jina la Bwege amesema yeye anaunga mkono tozo ya miamala ya simu iliyopitishwa na Bunge kuanza kufanya kazi hivi karibuni kwani makusanyo yatasaidia kutanua wigo wa kupeleka huduma muhimu kwa wananchi na kwa haraka.

Bwege amesema hayo leo Alhamisi, Agosti 5, 2021 wakati akihojiwa na kipindi cha Front page cha Global Radio huku akishauri kuwa tozo hizo zinatakiwa zipunguzwe ili wananchi waweze kulipia bila malalamiko.

“Tozo ya Miamala ya Simu naunga mkono lakini kubwa, lile jambo ni muhimu tozo ipunguzwe tu. Iwekwe kwenye mfuko maalum na kila mwezi watuambie wamekusanya Shilingi ngapi na kiasi gani wamepeleka kwenye huduma eneo gani kama ni Kilwa.

“Hata hii katiba tuliyo nayo kuna mambo ambayo hayasimamiwi vizuri, tukipata katiba mpya tutajua sasa tumesema hiki, huyu akienda kinyume tutajua namna ya kupambana naye, lakini katiba sio suluhisho kwa nchi ninavyoiona.

“Chadema wanadai Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi, sisi ACT Wazalendo tunataka tuanze mikutano ya hadhara, jino kwa jino hiyo. Katiba hii hii iliyopo iheshimiwe, nampenda sana Mama Samia, ninamuelewa sana na ninamkubali vilevile, lakini ninamuomba akae na wanasiasa, sababu hawa wanasiasa wanaweza kuiacha nchi salama ama wakaiharibu,” amesema Bungara (Bwege).

Chanzo: globalpublishers.co.tz