Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Butiku awapa somo viongozi

48705 Butiku+pic

Tue, 26 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mbeya. Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku, amesema ombwe la baadhi ya viongozi nchini kufanya kazi kwa matamko linatokana na kutofuata sheria na kutosoma katiba ya nchi inayotoa mwongozo wa kiongozi kila nafasi.

Butiku alisema hata kama wanasoma sheria na katiba hawaifuati kwa makusudi.

Alisema hayo jana kwenye ukumbi wa Mkapa akitoa mada kuhusu uongozi shirikishi kwa kuzingatia taratibu za kitaasisi inayowashirikisha wananchi wote kujiletea maendeleo yao.

Mdahalo huo uliandaliwa na taasisi yake kwa kuwashirikisha viongozi mbalimbali mkoani hapa.

Batiku aliongeza kuwa kwa sasa nchi imepoteza muelekeo wa kuandaa midahalo ya kujadili maendeleo kwa kushirikisha vyama vya siasa ndiyo chanzo cha kushindwa kuruka kihunzi cha maendeleo kwa wananchi.

Akizungumza kwenye mdahalo huo mkuu wa mkoa wa Mbeya Albert Chalamila, alisema dhana ya uadilifu na uzalendo kwa viongozi na watumishi wa umma wanatakiwa kufanyia mazoezi kila mara wakati wa utekelezaji majukumu yao.

Chalamila alisema viongozi wengi wamekuwa wakihimiza wananchi kuwa wazalendo lakini wao hawatekelezi kwa vitendo dhana ya uadilifu na uzalendo.

Naye kaimu katibu tawala mkoa wa Mbeya Jelemiah Minja, alisema kwa kutumia dhana shirikishi kwa wananchi mkoa umefanikiwa kujenga sekondari 14.

“Katika Mkoa wangu tunajidai kwa sababu wananchi wanajitambua kufanya shughuli za maendeleo ambazo zinawakabili, kufikia Februari mkoa unadaiwa zaidi ya Sh7.8 bilioni kukamilisha maboma ya vituo vya afya na zahanati na tunarajia kuzipata kwenye bajeti mwaka wa fedha ujao,” alisema.



Chanzo: mwananchi.co.tz