Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

‘Bunge linauma na kupuliza’

Bungeni 660x400 1 ‘Bunge linauma na kupuliza’

Thu, 9 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wadau wamedai kuwa bado Bunge la Jamhuri ya Muungano halina uwezo wa kuiwajibisha Serikali na badala yake linang’ata na kupuliza,

Wamewataka wabunge wa Bunge la Tanzania kuwasemea wananchi bila woga hasa katika uchambuzi wa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na kuacha kuuma na kupuliza.

Hayo yamesemwa leo Jumatano, Novemba 8, 2023 na Mwenyekiti wa Vijana Chama cha NCCR Mageuzi, Nicholaus Gaboni wakati akichangia mada ya Mwananchi X Space inayosema “Nini kitarajiwe kuhusu ripoti ya CAG baada ya maazimio ya Bunge?”

Amesema bado kuna changamoto kwa wabunge kushindwa kuwa wawazi kuwataja hadharani wabadhirifu.

“Bunge linauma na kupuliza. Kuna Mbunge mmoja (hakumtaja) alisema kuna wabadhirifu wengiu na Jumatatu atawataja wezi wote, leo ni Jumatano hajafanya alichosema. Tuna mifumo inayolea wezi, wabadhirifu na wezi wa fedha zetu. Masikini wa nchi hii ambao wanavuja jasho fedha yao itumike vizuri kwa nguvu zetu. Marehemu Rais (John) Magufuli alitusaidia sana angalau watu waliogopa,” amesema Gaboni.

Kwa upande wake msemaji wa sekta ya utawala bora kutoka Chama cha ACT Wazalendo, Pavu Abdallah amesema waliohusika na ubadhirifu ni watendaji katika serikali na katika dhana ya utawala bora vitu vingi vimekosekana.

Amesema kutokuzingatiwa kwa kanuni, taratibu na miongozo pamoja na misingi ya haki na usawa viongozi wengi wanashindwa kuzingatia haki na usawa na wengi wanaangalia maslahi yao binafsi.

“Wizi wa mali ya umma hata CAG ameeleza kwa kina kabisa, unyanyasaji wa wananchi, kukosekana uwazi na uwajibikaji baada ya kutokea yote yaliyotokea wananchi wanataka kuona hatua kali zinachukuliwa kwa wote walihusika na kadhia hii,” amesema.

Amesema ripoti zimekuwa zikitolewa lakini hazionyeshio wahusika kuchukuliwa hatua na kwamba wananchi wanapenda kuona mabadiliko yanatokea katika maeneo mbalimbali.

Naye mchangiaji Clay Mwaifani amaesema ni wajibu kwa serikali kuona namna gani wanalitekeleza agizo la Bunge.

“Taifa letu linateswa na watu wanaoweza kufanya lolote na wasifanywe chochote. Watu ambao wamekuwa wakitajwa kwenye ripoti za CAG hawawajibiki sasa ni nani anatakiwa kuwawajibisha.

“Kama hatuwezi kumshtaki Rais itatuwia vigumu kuwashtaki hawa watendaji wengine ambao wanafanya kazi kwa niaba yake na ndiyo hao wanaotajwa kwa ubadhirifu kwenye ripoti za CAG,” amesema Mwaifani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live