Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bunge latoa neno kifo cha Mbunge wa ACT Wazalendo

MBUNGEEEEEEEE Bunge latoa neno kifo cha Mbunge wa ACT Wazalendo

Thu, 20 May 2021 Chanzo: eatv.tv

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeahirisha vikao vyake vya leo mpaka kesho tena kufuatia kifo cha mbunge wa jimbo la Konde kupitia Chama cha ACT Wazalendo Khatib Haji, aliyefariki dunia alfajiri ya leo katika hospitali ya Taifa Muhimbili.

Submitted by Agnes Kibona on Alhamisi , 20th Mei , 2021 Marehemu Khatib Haji, aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Konde kupitia Chama cha ACT Wazalendo.

Akitoa taarifa ya msiba huo leo Mei 20, 2021, Bungeni Dodoma, Naibu Spika wa Bunge hilo Dkt. Tulia Ackson, amesema kuwa mbunge huyo amefariki wakati akipatiwa matibabu na mazishi yanafanyika leo saa 10:00 jioni huko visiwani Pemba.

"Mh. Spika kwa masikitiko makubwa anawatangazia waheshimiwa wabunge kwamba mbunge mwenzetu Khatib Haji, mbunge wa jimbo la Konde kupitia Chama cha ACT Wazalendo, amefarikia dunia alfajiri ya leo katika hospitali ya Taifa Muhimbili na mazishi yatafanyika leo Pemba, tutawakilishwa na wabunge wenzetu walioko Dar es Salaam", ameeleza Dkt Tulia Ackson

Chanzo: eatv.tv