Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bunge lapunguza wageni, lasitisha ziara za mafunzo

6efd191d4c3cad8e330a500e0e7fb9e5 Bunge lapunguza wageni, lasitisha ziara za mafunzo

Sat, 10 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

BUNGE la Tanzania limesitisha ziara za mafunzo kwa wanafunzi na makundi mengine ikiwa ni hatua ya kuepuka msongamano wakati wa Bunge la 12 Mkutano wa tatu unaoendelea kwa sasa.

Sambamba na hao, pia wizara itatakiwa kupeleka bungeni watendaji wasiozidi 15 ili kusaidia wakati wa Bunge la Bajeti wakati bajeti husika wizara itakapokuwa inawasilishwa na kujadiliwa.

Naibu Spika Dk Tulia Ackson alitoa mwongozo huo jana wakati akisoma tangazo lililotolewa na Katibu wa Bunge, Stephen Kigaigai.

Dk Tulia alisema Ofisi ya Katibu wa Bunge imeweka utaratibu huo kwa ajili ya kulinda afya za wabunge pamoja na watumishi katika kipindi hiki cha Bunge la Bajeti ambacho wamekuwa wakipokea wageni wengi, hivyo msongamano unakuwa ni mkubwa.

“Utaratibu umewekwa lengo lake ni kudhibiti msongamano wa wageni bungeni lakini kwa ajili ya kulinda afya za wabunge na watumishi wa Bunge,” alisema Dk Tulia.

Alisema wabunge wataruhusiwa kupeleka wageni bungeni wasiozidi watano kwa kibali maalumu cha Ofisi ya Katibu wa Bunge.

Katika mwongozo huo, mbunge atatakiwa kupeleka maombi yake katika ofisi hiyo ambayo wataangalia ni wageni wangapi wapo kwa siku na kama watapata nafasi siku hiyo.

Alisema wizara itatakiwa kupeleka bungeni watendaji wasiozidi 15 ili kusaidia wakati wa Bunge la Bajeti wakati bajeti husika ya wizara ikiwasilishwa na kujadiliwa.

“Ziara za mafunzo kwa wanafunzi na makundi mengine ya jamii zimefutwa. Waheshimiwa wabunge tutoe ushirikiano,” alisema.

Chanzo: www.habarileo.co.tz