Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, jana Aaprili 13, 2023 lilijadili na kuipitisha Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu bungeni jijini Dodoma.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipongezwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama baada ya Bunge kupitisha Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu ya 2023/2024.
Wengine waliompongeza ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi na Waziri wa mambo ya Nje ya Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Stagomena Tax.