Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bunge lanusa harufu ya mishahara hewa

Bunge Pic Data Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Thu, 17 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC) imebaini viashiria vya kuibuka tena kwa mishahara hewa Serikali baada ya kiasi cha mishahara kutoka Hazina kutofautiana na mahitaji halisi ya mishahara katika mfumo wa Lawson.

Hayo yamesemwa leo Alhamis Februari 17, 2022 na Mwenyekiti wa LAAC, Grace Tendega wakati akiwasilisha taarifa ya shughuli za Kamati hiyo katika kipindi cha Januari 2021 hadi Februari 2022.

Ametoa mfano wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo ambapo mahitaji ya Lawson ilikuwa ni Sh13.16 bilioni lakini Hazina ilitoa Sh13.30 bilioni na hivyo kusababisha ziada ya Sh145. 73 milioni.

Amesema kwa upande wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua mahitaji ya Lawson yalikuwa ni Sh17.67 bilioni lakini Hazina ilipeleka Sh17.88 bilioni hivyo kuwa na ziada ya Sh209 milioni.

Ametaja pia Halmashauri ya Wilaya ya Uyui mahitaji ya Lawson yalikuwa Sh17.06 bilioni lakini Hazina ilipeleka Sh17. 37 bilioni na ziada ya Sh309.34 milioni.

“Hoja hii inaashiria kwamba serikalini kuna usimamizi hafifu wa mfumo wa mishahara. Udhaifu huu usipodhibitiwa utaibua upya mishahara hewa serikalini,” amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live