Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bunge laitaka serikali kuchunguza maduka makubwa

56d40c30834cec298e874396e1405c98 Bunge laitaka serikali kuchunguza maduka makubwa

Wed, 16 Jun 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MWENYEKITI wa Bunge, Mussa Zungu ameitaka serikali kupeleka wataalamu kuchunguza bidhaa hasa za sabuni katika maduka makubwa (supermarket) kwa madai kwamba bidhaa nyingi ni bandia.

Akiongea bungeni Juni 16, 2021, Zungu alidai kuwa sabuni nyingi hasa zenye majina makubwa ni bandia akitolea mfano sabuni ya Dettol.

Zungu ambae pia ni Mbunge wa Ilala (CCM) alisema “ukiweka Dettol kwenye maji inakua nyeusi. Tumeni watuweni kwenye supermarket makubwa, Dettol, na sabuni za kuogea zote feki. Watu wanalipa pesa nyingi wanatumia vitu sio halali na pesa wanazolipa. Chunguzeni supermarket zote.”

Hata hivyo, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe amesema serikali inakusudia kutunga sera na sheria ya kumlinda mlaji.

Chanzo: www.habarileo.co.tz